Serikali imefuta usajili wa magazeti 473 ambayo hayajachapishwa kwa kipindi cha miaka mitatu.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo,  Nape Nnaye

Hatua hiyo imetangazwa leo na Waziri wa Habari, Nape Nnauye katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Ukumbi wa Maelezo.

Amesema mtu yeyote atakayechapisha magazeti hayo kwa njia ya nakala ngumu (Hard copy) au kielektroniki atachukuliwa hatua za kisheria.

“Iwapo kuna mmiliki wa gazeti ambaye angependa kuendelea na biashara hii milango iko wazi kwa ajili ya kuwasilisha maombi mapya sio kuuhuisha yaliyofutwa,” alisema Nape.


Post a Comment

 
Top