• Breaking News

  Jul 31, 2016

  Vijana Waonywa Kurubuniwa na Wanasiasa


  Umoja wa vijana chama cha mapinduzi – UVCCM umewataka vijana kutokubali kurubuniwa ama kutumiwa na wanasiasa kwa maslahi yao binafsi badala yake wajikite katika kuchangia suala la kuleta maendeleo hapa nchini.

  Wito huo umetolewa jijini Dar es salaam na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Abdul Shaka wakati akizungumza na waandishi wa habari mambo mbalimbali ya jumuiya hiyo, ambapo pia amewaonya vijana kutoshiriki kwenye oparesheni Ukuta itakayoendeshwa na Chadema ambayo amedai inalenga kuvunja amani.

  Aidha amezungumzia mikakati itakayokwenda kutekelezwa na jumuiya hiyo kuwa ni kuyarudisha majimbo yote yaliyochukuliwa na upinzani jijini dar es salaam ifikapo mwaka 2020.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku