Mtwara. Idara ya uhamiaji mkoani Mtwara imewakamata wahamiaji haramu 18 raia wa Ethiopia kwenye kijiji cha Kilambo, Mtwara Vijijini wakijiandaa kuvuka mpaka kwenda Msumbiji.

Kamishna msaidizi wa idara ya uhamiaji na ofisa uhamiaji Mkoa wa Mtwara, Rose Mhagama amesema wahamiaji hao wamekamatwa Jumatatu asubuhi wakiwa na hati za kusafiria, lakini hawakuwa na kibali cha kuingia nchini wala nchi wanayokwenda.


Post a Comment

 
Top