• Breaking News

  Jul 28, 2016

  Watumishi zaidi ya 50 jiji la Arusha kufukuzwa kazi kutokana na uzembe na udanganyifu.


  Watumishi zaidi ya 50 wa halmashauri ya jiji la Arusha wamechukuliwa hatua za awali na huenda wakafukuzwa kazi kutokana na uzembe na udanganyifu ukiwemo wa kutoa taarifa za uongo za utekeezaji wa miradi.

  Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi wa jiji la Arusha Bw Athumani Juma Mhamia amesema tatizo ni kubwa zaidi kwa watendaji wa idara ya fedha na mipango miji na idara ya usafi.

  Aidha Bw Mhamia amesema pia halmashauri hiyo inakabiliwa na tatizo kubwa la mtandao wa kuuza kujenga maeneo ya wazi na amewataka wote wanaojijua kuwa wanahusika kujisalimisha kwani hakuna atakayepona.

  Kuhusu tatizo la kukithiri kwa uchafu meya wa jiji la Arusha Bw. Kalst  Lazaro amesema tatizo kubwa ni ukosefu wa vitendea kazi na kwamba  halmashauri imenunua magari sita ya kuzolea taka ambayo yanatarajiwa  kupunguza tatizo hilo kwa kiasi kikubwa.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku