• Breaking News

  Aug 29, 2016

  UKWELI Kuhusu Freeman Mbowe Kuahirisha Operesheni UKUTA Septemba 1

  Freeman Mbowe
  CHADEMA inapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu andiko linalosambazwa mitandaoni likimnukuu Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe kuwa ameahirisha Operesheni UKUTA na maandalizi ya Septemba 1.

  Tunaomba umma upate taarifa sahihi kuwa Mwenyekiti Mbowe hajafanya mkutano na waandishi wa habari mahali popote pale kuzungumzia kuahirisha Operesheni UKUTA inayoendela nchi nzima wala kuzuia maandalizi ya Septemba 1.

  Kupitia taarifa hii, chama kinawataka viongozi, wanachama, wafuasi, wapenzi na mashabiki wa CHADEMA na Watanzania wote wazalendo na wapenda haki, kupuuza andiko linalosambazwa mitandaoni .

  Msisitizo unaendelea kutolewa kuwa Operesheni UKUTA ambayo imelenga kusimamia utawala unaoheshimu Katiba ya Nchi na kulinda sheria na maandalizi yanaendelea nchi nzima.

  Imetolewa na;

  Tumaini Makene
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
  CHADEMA

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku