• Breaking News

  Aug 5, 2016

  Ajali za Pikipiki Janga..Hospitali ya Moi Kupokea Majeruhi 40 Kila Siku wa Ajali za Boda Boda

  Meneja Uhusiano na Ustawi wa Jamii wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI), Jumaa Almasi amesema kwa siku wanapokea wagonjwa 40 wengi wao wakiwa majeruhi wa ajali za bodaboda.

  Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuitaka taasisi hiyo kurejesha kambi za upasuaji ili kupunguza idadi ya wanaosubiri upasuaji.

  “Awali walikuwa 20 kwa siku, lakini kwa sasa ni 40 na asilimia 80 ya wagonjwa hao wanahitaji upasiaji wa dharura na kiutaratibu, mwenye dharura anahudumiwa mapema ili kuokoa maisha,” amesema huku akisisitiza kuwa taarifa zilizoripotiwa kuhusu msongamano huo na kubana matumizi siyo za kweli.

  Lakini wakati Almasi akisema hayo, juzi, Waziri Ummy alifanya ziara ya kushtukiza MOI na kuagiza kambi za upasuaji zilizokuwa zikifanyika mwishoni mwa wiki zirudi mara moja ili kupunguza idadi ya wagonjwa wanaosubiri upasuaji.
  SHARE THIS

  Share on FacebookTweet on TwitterPlus on Google+

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku