Mkali wa wimbo ‘Aje’ AliKiba amekanusha taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa atafanya show katika utowaji wa tuzo za Uganda Entertainment Awards.
Katika mitandao ya kijamii zinasambaa banner ambazo zinamuonyesha AliKiba atakuwepo kwenye utowaji wa tuzo hizo ambazo inafanyika weekend hii.

Muimbaji huyo amesema yeye pamoja na uongozi wake hawana taarifa yeyote kuhusu show hiyo.

“Napenda kuwajulisha ya kuwa sitokuwepo wala kufanya show kwenye hafla ya tuzo za Uganda Entertainment Awards wikiendi hii jijini Kampala,Uganda!,” aliandika AliKiba facebook “Katokana na kutokuwa na mkataba na hao waandaaji wala mawasiliano nao, mimi binafsi wala uongozi,”

Aliongeza, “Akhsanteni mashabiki wangu wote wa Uganda na Africa Mashariki kwa mapenzi yenu, Na kwa kuniulizia kama nitakuwepo kwenye kutumbuiza siku hiyo. Nawaahidi tutaonana wakati mwingine hivi karibuni. Asanteni#KingKiba,”


Post a Comment

 
Top