Aug 20, 2016

Arusha Wataka Mkuu wa Mkoa Aachwe Afanye Kazi

WAKATI Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akiapishwa jana Ikulu, Dar es Salaam, baadhi ya wananchi wa Jiji la Arusha wameshangazwa kuona viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakidai kuwa anaingilia kazi za jiji hilo.

Mkazi wa jiji hilo, Ismail Isaac alisema tatizo ni siasa za chuki kati ya Chadema dhidi ya RC Gambo na kutaka wamuache afanye kazi kwani wananchi wanamkubali, hivyo kama chama hicho cha upinzani hakimkubali, kitajua chenyewe.

“Wananchi wanahitaji maendeleo sasa huu ushawishi wa Chadema kwenda kwa wenyeviti wa mitaa unatoka wapi? Huyu Gambo anafanya kazi, sasa vikwazo ni vya nini?” Alihoji Isaac na kusema kuwa Chadema inapaswa kutumikia wananchi na si maneno.

Aidha, alimpongeza Rais John Magufuli kwa kumteua Gambo.

Aliwashangaa madiwani wa Chadema wanaotaka siasa za chuki ambazo wananchi hawapo tayari kuzikubali. Kwa upande wake, Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Arusha, Shaaban Mdoe, alisema Arusha kuna siasa nyingi hivyo ni vyema viongozi wakatimiza majukumu yao ya kikazi na kutokatishwa tamaa

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR