Aug 25, 2016

Askofu wa zamani wa Afrika Kusini Desmond Tutu alazwa hospitali

Desmond Tutu 
Askofu wa zamani Desmond Tutu na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel kutoka Afrika Kusini, amelazwa hospitalini kwa mara nyingine tena baada ya kupata maambukizi.

Kupitia taarifa, wakfu wake umesema: “Anatarajiwa kusalia hospitalini kwa wiki moja au mbili. Askofu huyo alifanyiwa matibabu kama hayo mwaka uliopita.”

Haijabainika ni maambukizi ya aina gani ambayo mtetezi mkuu wa haki za binadamu na aliyepinga utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini amepata.

Familia yake imesema maambukizi hayo hayahusiani na saratani ya tezi dume ambayo imekuwa ikimtatiza kwa takriban miaka 20.

Askofu Desmond Tutu, 84, amekuwa akilazwa hospitalini mara kwa mara katika miaka ya hivi karibuni na amekuwa akitibiwa maradhi ya saratani ya tezi dume.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR