• Breaking News

  Aug 9, 2016

  BAVICHA: Hatumjaribu Rais Magufuli, tunasaidia kuonesha udhaifu wa serikali

  Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), limesema kamwe wanachama wake hawatashiriki kumjaribu Rais Dkt John Magufuli, bali watasaidia kuonesha upungufu uliopo ndani ya serikali.

  Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, Patrobas Katambi wakati akitoa tamko la kuunga mkono azimio la Baraza Kuu la Chadema juu ya kufanya maandamano nchi nzima Septemba Mosi, mwaka huu.

  “Hatutaki kumjaribu Rais na haya tunayoyafanya ni katika kuunga mkono utekelezaji wa majukumu yake kwa kumuonesha upungufu katika serikali, ”alisisitiza mwenyekiti huyo.

  Alisema kuwa kuhakikisha kuwa hatumjaribu Rais Magufuli kama ambavyo Rais alitahadharisha hivi karibuni na kwamba watafuata taratibu zote kisheria kuomba vibali vya kufanya mikutano hiyo.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku