Aug 7, 2016

Bavicha yaunga Mkono Ukuta

Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) limetangaza kuunga mkono azimio la Kamati Kuu la kufanya mikutano nchi nzima kuanzia Septemba mosi, mwaka huu.

Akizungumza na vyombo vya habari, Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi amesema watafuata taratibu zote za kisheria ikiwamo kutoa taarifa na kuomba ulinzi wa polisi.

Katambi amesema ajenda za mikutano hiyo zitakuwa ni kupinga ukandamizaji wa demokrasia nchini, pamoja na kupinga hatua ya viongozi wa vyama vya siasa kukamatwa na polisi mara kwa mara bila sababu za msingi.

"Wote tunaona jinsi Serikali inavyoingilia mihimili mingine. Mahakama ndiyo chombo pekee ambacho kinatoa haki, kama mhimili huu unaingiliwa basi hata hukumu zinazofanyika zitakuwa za mashaka," amesema Katambi.
Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR