• Breaking News

  Aug 10, 2016

  Bifu lazuka Kati ya The Rock na Vin Diesel Kwenye Utengenezaji was Fast 8


  Wiki hii The Rock aliwashtua mashabiki wake kwa kuandika kwenye Instagram kuwa baadhi ya waigizaji wenzake wa kiume kwenye filamu ya Fast 8 wana mambo ya kipuuzi.

  Haikujulikana hasa alimlenga nani na sasa imebainika kuwa mbaya wake ni muigizaji mkuu wa filamu hiyo, Vin Diesel ambaye pia ni producer.
  Inasemekana kuwa jitihada za kuwapatanisha wawili hao zinafanyika. Mara ya mwisho wawili hao walizichapa vikali kwenye filamu hiyo na sasa ugomvi huo umeingia kwenye maisha ya kweli, kwa mujibu wa TMZ. Uadui huo unaweza kuwa hatari kwa filamu hiyo. “The Rock’s rant about unprofessional male co-stars was targeted at Vin Diesel,” waliandika TMZ.
  Tovuti hiyo imeripoti kuwa wawili hao walikuwa na mkutano wa siri Jumanne hii kujaribu kuyamaliza. Inasemekana kuwa wawili hao walikorofishana kutokana na Vin ambaye ni producer pia kuchukua maamuzi ambayo The Rock hakukubaliana nayo. “Our sources say The Rock and Vin had a meeting on the Atlanta set mid-day Tuesday ... partly because tensions were running so high it was almost impossible to shoot scenes. We do not know if they resolved their issues,” wameandika TMZ.

  TMZ awali waliripoti kuwa waigizaji wengi wa filamu hiyo walichukizwa na ujumbe wa The Rock kwakuwa iliwafanya wote wakisiwe wamelengwa.
  Chanzo kimoja pia kimeiambia E! News kuwa utengenezaji wa Fast 8 umekuwa mgumu hasa kwa The Rock. “Things on set just ‘didn't feel exactly the same’ this time around. And while Johnson ‘is the best guy on the planet to work with,’ he’s ‘also a very emotional guy’ and ‘likes things to go as he sees fit [while] also being fair,’” kilisema chanzo hicho.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku