Aug 9, 2016

Bondia wa Namibia Akamatwa kwa Tuhuma za Ubakaji Rio Brazil Kwenye Michezo ya Olimpiki


Bondia wa Namibia ambae anashiriki michezo ya olimpiki huko Rio nchini Brazil, amekamatwa kwa tuhuma za kesi ya ubakaji. Jonas Junias ambae alibeba bandera ya Namibia siku ya ufunguzi wa michezo hiyo amepelekwa katika moja ya megereza makubwa huko mjini Rio.

Polisi wa Brazil wanasema alimbusu mhudumu wa chumba kwa lazima katika kambi ya wanamichezo na alimuahidi kumpa pesa kama atakubali kufanya nae mapenzi. Bondia wa Morocco Hassan Sada nae alikamatwa Ijumaa iliyopita. alikanusha tuhuma hizo lakini bado yupo chini ya usimamizi wa polisi.


Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR