Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye leo Agosti 11.2016, ametangaza rasmi kulifungia gazeti la MSETO kwa miezi 36 lisichapishe Habari zake hapa nchini kwa njia yoyote ile kutokana na kukiuka maadili ya taaluma ya Habari.


Waziri Nape Nnauye ametoa tamko hilo huku akizitaja tuhuma mbalimbali zikiwemo:  Uchochezi, Uongo na Upotoshaji ambapo hazizingatii kanuni za taaluma ya uandishi wa habari.


 Amri hiyo ya kulifungia gazeti la mseto imetokana na tangazo la Serikali namba 242 la tarehe 10/8/2016 kwa mujibu wa sheria ya magazeti ya mwaka 1976 sura 229 kifungu cha 25(1)


Aidha, Waziri Nape amesema gazeti hilo linaandika habari na taarifa za uongo ambazo zina nia ya kupotosha jamii ikiwa ni pamoja na kutumia nyaraka za serikali ambazo zimegushiwa ili kuwachafua viongozi wa serikali na seerikali yao.


Post a Comment

 
Top