• Breaking News

  Aug 3, 2016

  Chadema Wathibitisha Hapa Tundu Lissu Kumamatwa na Polisi Singida...

  Ujumbe toka CHADEMA:

  Ni kweli. Tunaweza kuthibitisha kwa vyombo vya habari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Chama Mh. Tundu Lissu anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Singida kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi.

  Polisi wamemkamata jioni hii baada ya kumaliza mkutano wake wa hadhara alioufanya Ikungi jimboni kwake kwa kile walichosema kuwa ni maelekezo kutoka juu hivyo anapaswa kwenda Kituo Kikuu cha Polisi Mkoani Singida. Taarifa kutoka kwenye mfumo wa chama mkoani humo zimesema muda mfupi uliopita ndiyo amewasili kituoni hapo na kupelekwa Ofisi ya RCO Singida.

  Tayari viongozi wa chama mkoani humo wako katika eneo hilo ili kuhakikisha Lissu anapata haki zake kama inavyostahili huku pia chama ngazi ya taifa, hususan Ofisi ya Katibu Mkuu, ikifuatilia kwa ukaribu kujua sababu hasa ya kushikiliwa kwake na kutoa msaada wa haraka kadri itakavyohitajika. Tutaendelea kuwajuza kuhusu suala hili.

  Makene​

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku