Aug 14, 2016

Daktari Asimamishwa Kazi Kwa Ulevi Kongwa


Dodoma. Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deogratius Nejembi amewasimisha kazi daktari mmoja na matabibu wawili wa Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa tuhuma za uzembe na ulevi.

Akizungumza na uongozi wa Mji Mdogo wa Kibaigwa, Ndejembi alisema alikwenda katika hospitali hiyo ya wilaya usiku akakaribishwa na Televisheni iliyokuwa inawaka.

“Nilikaa pale kwa muda wa dakika 45 ndio akatokea mtumishi akasema kuwa alikuwa katika wodi ya watoto. Lakini unajua tu ipo shida,”alisema.

Alisema kesho yake aliitisha kikao na maazimio yakawa kwamba daktari hayo asimamishwe kazi wakati uchunguzi ukiendelea.

Aliwataja waliosimamishwa ni daktari wa Meno, Dk Waziri Majuto ambaye amesimamishwa kwa ulevi na matabibu wawili  Daniel Ndahani ambaye alisimamishwa kwa kukosa weledi wa kazi na Denis Msovero hakuwepo kazini wakati alipoenda katika hospitali hiyo.


Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR