Aug 18, 2016

Dodoma Kuipeleka Tanzania Kwenye Uchumi wa Kati

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi inayojishughulisha na Utafiti Masuala ya Uchumi, Umaskini na Maendeleo nchini (REPOA) Dkt. Donald Mmari amesema kuwa, zoezi la kuhamishia serikali mkoani Dodoma litachangia kuongeza wigo wa biashara za aina mbalimbali

jambo litakalosaidia uchumi wa nchi kupanda na kufikia nchi ya kipato cha kati.

Akiongea katika mahojiano maalum aliyofanya na EATV Dk. Mmari pia ameshauri kuwe na mpango madhubuti wakuhakikisha mji unakuwa katika hali nzuri ya mipango miji, ushirikishwaji wa sekta binafsi ili zishiriki kikamilifu kwa kupewa motisha na mazingira rafiki ambay yatawasaidia katika kuwekeza kwenye sekta mbalimbali ambazo ni muhimu kwa mji ambao ni makao makuu ya serikali.

Aidha, Dkt. Mmari amesema licha ya mkoa huo kuwa na hali ya ukame, mazao yanayolimwa katika eneo hilo yanaweza kubadilisha hali ya uchumi kwa mkoa huo.

Tafiti za mwaka 2012 zilizofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) zinaonesha kati ya mikoa 25 iliyofanyiwa tafiti, mkoa wa Dodoma unashika nafasi ya 12 kwa umasikini.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR