• Breaking News

  Aug 18, 2016

  Epuka Sana Kuwa na Mwanaume Kapuku, Mnuka Vumbi.....

  Mwanaume ambaye hana kitu kabisa yaani negative muepuke sana tena ukikutana naye ana umri kati ya 25+, 30+ halafu hajiwezi, hutegemea watu wengine kwa kula kulala, bili za umeme,maji n.k anategemea zilipwe ni heri ukutane na COBRA porini huyo ni hatari  

  Unakuta mwanaume kasoma hadi chuo, form six n.k lakini hajishughulishi kwa lolote anaishi kwao, kwa ndugu, kwa marafiki kajipiga sopusopu tu na ana afya njema anacheka hadi jino la mwisho hashtuki kimbia umelamba dume!

  Hebu jiulize mwanaume ambaye hajiwezi yeye mwenyewe unategemea akupe msaada gani katika kulea watoto endapo mtaoana? analishwa, kodi hajui kuisotea hajui kukuru kakara za wenye nyumba unategemea atawaza kujenga? sahau!

  Utamkuta busy kuponda kazi za wenzake na kuziona ni mbaya ni za hali ya chini yeye ndo mjanja hafanyi kazi za kifala, anajisemea kikazi cha laki 3 sifanyi huku akiambiwa asimamie show ya tumbo lake tu semister moja anachemka!

  Hivi hadi vibarua vya kawaida hawezi kufanya akapata chochote walau akawa na maisha yake ya chini ya kuanzia, kubeba zege, mbogamboga, matunda n.k hawezi kuuza?

  Kiufupi ukiona mtu mzima ni tegemezi usitegemee mazuri wana tabia hizi:


  • Hawajiamini(ugomvi kila mara)
  • Huwa wababe sana walau
  • Huonesha uanaume wao
  • Hawana shukurani hata wafanyiqe nini kulalamika tu.
  • Hawawakubali watu wengine huponda kila kitu.
  • Hata akikosea haombi msamaha anahisi samahani ni umasikini
  • Mkihitilafiana kidogo huunganisha na umasikini wake labda ndo maana mnagombana!
  • Hana tabia maalum akipata ka elf hamsini hilo gubu lake ni hatari
  • Kama ni mchumba akipata hela lazima akuache maana anahisi kwakuwa unajua historia yake hutamthamin (hawajiamini)
  Hebu olewa na kuwa na mtu ambaye ana chochote anajua bajeti ya kula ilivyo ngumu, " hamnaga mapenzi na njaaa"

  Kama unabisha Toa Maoni yako Hapa Chini Kwa Hoja....

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku