• Breaking News

  Aug 8, 2016

  Habari Njema Kwa Mashabiki wa Man United Kuhusu Usajili wa Mchezaji Paul Pogba Hii Hapa

  Headlines za kiungo wa kimataifa wa Ufaransa aliyekuwa anaichezea klabu ya Juventus ya Italia Paul Pogba kuhusishwa kujiunga na Man United, zinaelekea kumalizika kwa kiungo huyo kurudi Man United toka aondoke mwaka 2012.

  Leo August 7 2016 klabu ya Juventus ambayo ilikuwa inahitaji rekodi ya dunia ya usajili ya pound milioni 100 kama ada ya usajili wa staa huyo, imemruhusu staa huyo kufanya vipimo vya afya Man United.

  Pogba ambaye ana umri wa miaka 23 aliondola Man United 2012 na kujiunga na Juventus kwa dau la pound milioni 1.5, Pogba amefanikiwa kushinda mataji manne ya Ligi akiwa na Juventus. Pogba atakuwa staa wa nne kusaliwa Man United chini ya Jose Mourinho baada ya  Eric Bailly, Ibrahimovic na Henrikh Mkhitaryan.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku