• Breaking News

  Aug 4, 2016

  Hans Poppe : Sioni Tatizo Pesa za Okwi Kuwekwa Kwenye Akaunti ya Aveva Mbona Pesa ya Samatta iliwekwa Kwenye Akaunti ya Mke wa Rage


  Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema haoni kama kuna tatizo kwa uongozi wa Simba kuamua kuweka fedha zake kwenye akaunti ya mwenyekiti wake huku akisisitiza hata fedha za mauzo ya Mbwana Samatta, zilipitia kwenye akaunti ya aliyekuwa mwekiti wao wa zamani.

  Hans Poppe amesema, kama kweli Aveva alishikilia na kulazwa rumande eti kwa kuwa fedha za malipo ya Emmanuel Okwi dola 300,000 kutoka Etoile Du Sahel, basi anashangazwa sana.

  “Kweli hilo ni suala la mtu kushikiliwa hadi kulazwa ndani? Kama kweli suala ni hilo, basi ninaamini kutakuwa na tatizo jingine.
  “Fedha za Simba kupitia kwenye akaunti ya kiongozi wala si tatizo, mbona fedha za Samatta kutoka TP Mazembe zilipita kwenye akaunti ya (Ismail) Rage, sasa mbona hakukuwa na tatizo?” alisema Hans Poppe.

  Aveva alishikwa juzi na kulala katika kituo cha polisi cha Urafiki jijini Dar es Salaam, lakini kumekuwa na mkanganyiko kwa kuwa Takukuru, hawajasema lolote kuhusiana na kushikiliwa kwake ingawa taarifa zimezagaa kuwa ni fedha za malipo ya Okwi kuhamishwa kutoka kwenye akaunti ya Simba na kuwekwa kwenye akaunti yake.


  Inaelezwa, kwa pamoja walikubaliana kuziweka kwenye akaunti ya Aveva. Tayari, baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji pia wameitwa kuhojiwa ingawa haijajulikana ni akina nani.

  1 comment:

  1. Viongozi ni vibaya kama wa wafadhili. Mnafanya hivyo ndiyo sababu mnakopa benki na kama mnaindolewa madarakani fedha hazipo klabuni. White collar thieves.

   ReplyDelete

  Siasa

  Michezo

  Udaku