• Breaking News

  Aug 21, 2016

  Hatimaye, Prof Lipumba Aitwa Mkutano Mkuu

  Prof. Ibrahim Lipumba 
  Katika hali isiyo ya kawaida, Prof. Ibrahim Lipumba ameitwa kwenye Mkutano Mkuu wa CUF. Wajumbe wa Mkutano mkuu wamemshinikiza Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif amuite Lipumba kujieleza kwanini anajiuzulu ndo wafanye Uchaguzi.

  Hapo awali Baada ya kusomwa kwa barua ya kujiuzulu kwa Lipumba, wakapewa nafasi wajumbe waijadili. Kila Mjumbe aliyesimama alitaka Lipumba aitwe.

  Maalim Seif aliwambia hawezi kuitwa sababu alijiuzulu mwenyewe, wale wanaoitwa ni wale waliosimamishwa na Chama. Kumuoita ni kwenda kinyume na Taratibu na katiba ya Chama.

  Baada ya kusema hivyo, wajumbe wakasimama wote wakaanza kuimba hii ni dhuruma tunamtaka Lipumba...oooh chama..chama cha wananchi CUF.


  Mkutano ukaingia kwenye sintofahamu ndipo akaitwa Lipumba. Inaonekana hakuwa Mbali.
  Baadhi ya Wajumbe walihoji kwanini Prof. Lipumba ajiuzulu kwani Lowassa alijiunga CUF ? Nyumba ya Jirani inatuhusu nini?

  Profesa Lipumba aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho kikuu cha upinzani kuanzia 1995 hadi mwaka jana, aliachia ngazi kwa kile alichodai kupinga uamuzi wa viongozi wa vyama vinavyounda Ukawa kumpokea Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

  Baada ya profesa huyo wa uchumi aliyegombea urais mara nne kujiweka kando, CUF iliunda kamati ya watu watatu chini ya uenyekiti wa Twaha Taslima, kukiongoza chama hicho hadi hapo utakapofanyika uchaguzi mwingine wa viongozi.
  VIDEO:

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku