• Breaking News

  Aug 14, 2016

  Hivi ni Kweli Naibu Spika Hajamtembelea Spika wa Bunge Tangu Atoke Hospital?

  Kama ni kweli hapa kutakuwa na tatizo si bure. Sababu hatuwezi kusema ni ubusy sababu Tulia tunamuona kila siku akishiriki Vikao vya CCM na Warsha Mbalimbali.
  Kama mtu anayelalamika kunyang'anywa Urais Maslim Seif, Mwenyekiti wa CHADEMA Freema Mbowe, Kiongozi Mkuu wa ACT Zitto Kabwe na Wengine wengi wamemtembelea Spika kumpa pole, iweje yeye mfanyakazi mwenzie asiende?

  Hivi majuzi alikuwa analalamikiwa kwamba anafanya maamuzi bila kumshirikisha Spika. Alipeleka hundi ya shilingi bilioni sita zilizotolewa na Ofisi ya Bunge kwa kile alichodai alitekeleza kwa vitendo kauli ya kubana matumizi yasio na Tija ili fedha hizo zikanunulie madawati kwa ajili ya wanafunzi. Hii yote ilifanyika Spika akiwa Hospital kalazwa.

  Baada ya habari hii kusambaa, Spika na Wabunge walishangaa sana kuona hela inapelekwa Ikulu badala ya kupelekwa hazina. Hata hivyo walishangaa kwanini warudishe hela wakati Wabunge wanaidai bunge pesa nyingi tu? Hadi wabunge wameshindwa kwenda mafunzo kwa vitendo.

  Kitu kingine kilichomuumiza Spika ni hali ya kuruhusu wabunge wa chama kimoja CCM kwenda nje ya nchi huku wale wa vyama Vingine wakinyimwa ruhusa huku kila mtu akijua Nchi yetu na Bunge letu ni la vyama Vingi.

  Spika wa Bunge anaonesha manung'uniko yake waziwazi kwa Kitendo cha Naibu Spika kushindwa kumaliza mvutano uliopo kati yake na UKAWA ambapo ameahidi kulivalia njuga.

  Kingine ni kwamba kuna mvutano ndani ya wakubwa hawa kwa ile hali ya kila mmoja kujiona bora kuliko mwenzie.

  Je haya Mambo yanaweza kuwa ndo sababu ya naibu Spika kutomtembelea boss wake? Najiuliza sana. Kwani hii haileti picha nzuri kama imefikia hatua hii.

  Haya mambo yakiendelea tutakuwa hatujengi Taifa. Kwani hali kama hii inaleta mgawanyiko na chuki zisizo za lazima.

  Nashauri kila mmoja ajue nafasi yake ilipo. Kujipendekeza ili uonekane bora kuliko mwenzako haifai.

  Je ni kweli Tulia Ackson Hajamtembela Nyumbani kwake Spika wa Bunge Job Ndugai?

  By Figganigga/Jamii Forums

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku