• Breaking News

  Aug 26, 2016

  Hivi Steve Nyerere Bado Tunamuita Msanii?

  Kuna huyu bwana mdogo anaitwa Steve Mangere, siku za nyuma tulizoea kumwona katika majukwaa akimwigiza sauti hayati Baba wa Taifa, kutokana na hilo akaanza kujiita Steve 'Nyerere', hivi siku hizi anafanya nini, hivi na yeye bado tunamwita msanii?

  Huyu jamaa toka azimwe na wasanii wachanga wa kuigiza sauti, siku hizi hayupo kabisa kwenye Game badala yake amebaki kudandia dandia vitu tu hata asivyovijua hasa kwenye suala la Siasa za kutetea kile Chama cha Majipu, mara leo Kampeni, mara kageuka msemaji wa wasanii juu ya UKUTA, yaani UKUTA uliowashinda akina Kinana yeye ndo atauweza?!

  Alijaribu kuingia kwenye Maigizo mpaka wakampa na cheo cha Rais wa Bongo Movie lakini bado na kwenyewe kachemka, tuna haja gani ya kuendelea kumtambua kama Msanii?? Na toka wamnyime Ukuu wa Wilaya naona kama kavurugwa zaidi, au nyie mnamwelewa? Usanii umemshinda, Siasa haiwezi, apumzike tu Nyumbani, wakati mwingine hata kukaa kimya nayo ni Busara

  By Babu wa Kambo/JF

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku