• Breaking News

  Aug 3, 2016

  Huduma ya usafiri wa TRENI ya Pugu kutolewa bure mpaka Ijumaa Agosti 05

  Taarifa kutoka makao makuu ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), inaeleza kiwa huduma ya treni ya Pugu itaendelea kuwa ya majaribio hadi Ijumaa Agosti 5, 2016, hivyo abiria watakiwa kuendelea kujinafasi kwa huduma hiyo ya bure hadi siku hiyo.

  Hata hivyo kuanza rasmi kwa huduma hiyo kutategemea idhini ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi kavu na majini (Sumatra).

  Leo Jumatano Agosti 3, 2016 Wataalamu wa Sumatra walisafiri na treni hiyo na kutoa maagizo maalum ya kurekebisha mabehewa ya treni hiyo, na TRL imeshajiandaa kufanya marekebisho hayo kwa wakati muafaka.

  Treni ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) ikiwa tayari kwa safari yake ya Jiji kuanzia Stesheni  kwenda Pugu huduma ambayo imeanza kutolewa huku ikiwapa abiria nafasi ya kusafiri bure hadi Ijumaa Agosti 5, 2016

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku