Aug 27, 2016

Is January Makamba Political banned?

January  Makamba
Zinapita siku, wiki, miezi na hata mwaka unaisha sasa bila kumwona au kumsikia Kijana Machachari na makini Januari Makamba katika duru hizi za siasa ya awamu ya tano.
Kwa wanaomtambua Makamba wanaelewa uwezo wake wa kucheza na siasa za Tanzania kama alivyo Lowassa enzi za ujana wake. Ni kijana ambaye hutulia pale ambapo hupatwa na misukosuko a kisiasa na kujipanga upyaa. Pamoja na kwamba mimi ni moja ya watu wasioipenda CCM lakini Makamba ni hazina safi ambayo hata ukienda upinzani utampata mmoja au wawili wanaofanana naee.

Nakumbuka sote tulioshiriki katika uchaguzi wa mwaka jana tulivyo ona mipango ya ushindi wa Magufuli chini ya kijana huyu. Lakini sijui kimetokea nini mpaka kijana huyu machachari kupotezwa kwenye siasa na kutuipwa wizara mfu.

Niseme wazi kwamba pamoja na figisufigisu za kijana huyu mwaka jana lakini ni Hazina pekee ya mipango iliyosalia CCM. Hakuna kijana ambaye unaweza mfananisha na Makamba ndani ya CCM leo, sio Mwigulu wala Kigwangala. Huwezi msikia Makamba katika mihemko na mwendokasi wa hovyohovyo.
Najua wengi wanamlaumu Makamba kwa Bomoabomoa ya mabondeni ilivyofanyika, lakini ukweli ni kwamba bomoa bomoa ile ilifanywa na Lukuvi na Majaliwa.

Magufuli ameshindwa kumtumia Kijana huyu katika wizara kubwa hapa nchini na hii ndio inawezakuwa sababua kuyumba kwa serikali yake. Makamba alipaswa kuwa wizara ya Mambo ya nje au Waziri Mkuu.

Je huu ni mwanzo wa kufifia kwa Makamba katika siasa?
Makamba alikosa nini hasa kwa mtukufu Rais mpaka akapewa wizara ile?

Is makamba political Banned???

Karibuni kwenye mjadalaa, matusi, vijembe, hekima na busara ni haki yako, sio uchochezi.

By Ibilisi/JF

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR