Aug 9, 2016

ITV na Clouds Media vyatozwa faini ya Tsh 19M na TCRA

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia kitengo chake cha maudhui Jumanne hii kimevitoza faini ya jumla Sh19m vituo vya utangazaji, ITV, Clouds TV na Clouds FM kwa kukiuka kanuni za utangazaji.

TCRA wanasema Clouds Media imepigwa faini hiyo kutokana na kosa la kushabikia mapenzi ya mbuzi na binadamu kwenye chombo chao cha habari na kupiga wimbo wa mwanamuziki Mwana FA ambao unapaswa kupigwa muda maalumu ambao wameagizwa.

ITV wamepigwa faini hiyo kutokana na kipindi kutoka bungeni kilichokuwa kinaoongozwa moja kwa moja,ambapo Mbunge wa Iringa Mjini alisikika akisema “Naibu Spika amekuwa kama anavaa pampas,hataki kubanduka kwenye kiti kuongoza bunge”.

TCRA imewakumbusha wadau wote kufuata sheria na maadili ya utangazaji ili kuepuka adhabu na ukiukwaji wa maadili.

Source: Mwananchi/Jamii Forum

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR