• Breaking News

  Aug 15, 2016

  Je, Spika Ndugai yatamkuta kama yaliyomkuta Sitta 2010?

  Samwel Sitta ndiye amasemwa kuwai kuwa Spika bora kabisa katika Bunge la Tanzania !!
  Baada ya kufanya kazi Kwa weledi mkubwa kuanzia 2005-2010 wote muliona alivyofanyiwa figisu figisu mwaka 2010.

  Tuliambiwa 2010 kuwa ni zamu ya mwanamke hivyo tumuache Anna makinda aliongoze bunge !!!

  Tukamuacha akaongoza mpaka 2015 wote tuliona bunge lilivyompeleka puta mpaka akasalimu amri Kwa wakina Tundu Lissu !!!

  Wakaenda mbali zaidi watu wa mikakati ili kumaliza mvuto wake aliokuwa nao Kwa wananchi Samuel Sitta akapewa bunge la katiba ili alivuruge na kupoteza imani Kwa wananchi juu yake na walifanikiwa!!

  Mama makinda ni mjanja sana baada ya kuona heshima yake Kwa jamii itashuka ameamua kukaa pembeni na hili litamfanya aendelee kuheshimika Kwa jamii Tofauti na Sitta..

  Ndungai akaingia na Kwa jinsi inavyoonekana atafanya vizuri kuliko naibu wake !!

  Isingekuwa si kuugua nazani Ndungai angefanikisha Kwa weledi bunge la Budget .

  Lakini ninachokiona Ndungai atakuja kufanyiwa figisu figisu mwaka 2020 asirudi kuwa Spika Kwa kutumia njia hiyo hiyo iliyotumika kumkata Sitta 2010 na kumleta rasimi Tulia awe Spika na kazi ya kitengo itakuwa imefanikiwa!!

  Stay tuned!!

  SOURCE:Jamii Forums/technically

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku