• Breaking News

  Aug 22, 2016

  Jeshi la Polisi: Mazoezi Yanayoendelea ni ya Kawaida, Hayalengi Kuzuia Shughuli zozote Halali

  Taarifa ya Jeshi la Polisi Kwa Vyombo Vya Habari

  Katika siku za hivi karibuni, kumekuwepo na mitazamo tofauti miongoni mwa jamii kufuatia kuonekana kwa askari polisi wakifanya mazoezi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

  Kufuatia hali hiyo, jeshi la polisi nchini, linatumia fursa hii kuwatoa hofu wananchi kwamba mazoezi hayo ni ya kawaida kwa askari wa jeshi la polisi

  Aidha, jeshi la polisi linawataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kawaida kwa sababu mazoezi hayo hayalengi kuzuia shughuli zozote halali zinazofanywa na wananchi.

  Imetolewa na:
  Advera John Bulimba – Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP)
  Msemaji wa Jeshi la Polisi,
  Makao Makuu ya Polisi.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku