• Breaking News

  Aug 8, 2016

  Jose Mourinho na Man United Wafanya Kweli Kwa Kuifunga Leicester City na Kuchukua Ngao ya Jamiii

  Wiki moja kabla ya Ligi Kuu England kuanza huwa ni kawaida kuchezwa mchezo wa ngao ya jamii, mchezo ambao huzikutanisha timu Bingwa wa Ligi Kuu na Bingwa wa Kombe la FA, August 7 2016 England katika uwanja wa Wembley Leicester City ambaye ni Bingwa wa EPL na Man United ambaye ni bingwa wa FA walikutana.

  Huo ulikuwa mchezo wa kwanza wa mashindano kwa kocha Jose Mourinho aliyejiunga na Man United msimu huu sambamba na nyota Zlatan Ibrahimovic aliyetumia mechi hiyo kudhihirisha ubora wake wa kucheka na nyavu, katika mchezo huo Man United wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1.

  Man United walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 31 kupitia kwa Jesse Lingard ila Leicester City walisawazisha goli hilo dakika ya 52 kupitia kwa mshambuliaji wao aliyeng’ara msimu uliopita Jarmie Vardy, furaha ya Leicester City ilimalizwa na Zlatan Ibrahimovic dakika ya 83 na kuipa ubingwa wa Ngao ya Hisani.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku