• Breaking News

  Aug 21, 2016

  Joseph Kabila Uchaguzi Congo Wahairishwa, Kabila Kuongoza Hadi 2017

  Joseph Kabila
  Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imetangaza kuahirishwa uchaguzi wa rais nchini humo hadi mwezi Julai 2017.

  Habari hiyo ilitangazwa jana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Kongo, Corneille Nangaa na kuongeza kuwa, shughuli ya uandikishaji majina ya wapiga kura iliyoanza mwezi Machi mwaka huu, itachukua muda wa miezi 16 hadi kukamilika.

  Awali mahakama ya juu ya nchi hiyo ilitangaza kuwa iwapo serikali ya Rais Joseph Kabila haitaweza kuanda uchaguzi wa rais katika wakati ulioainishwa basi kiongozi huyo anaweza kubakia madarakani hadi wakati wa kufanyika uchaguzi mkuu.

  Kabila alishika hatamu za kuiongoza Congo mwaka 2001 baada ya mauaji ya baba yake, Laurent Kabila, na kisha akashinda uchaguzi wa rais uliofanyika mwaka 2006.

  Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Rais Joseph Kabila haruhusiwi kugombea tena kiti hicho baada ya kuongoza katika vipindi viwili vya Miaka 5 mfululizo.

  Na Regina Mkonde

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku