• Breaking News

  Aug 30, 2016

  JULIUS Mtatiro Ala Shavu, CUF Wamteua Kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Muda

  Julius Mtatiro
  Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF) limemteua Julius Mtatiro kuwa mwenyekiti wa kamati ya muda ya uongozi hadi utakapoitishwa mkutano mkuu maalumu mwingine baada ya ule wa awali kuvunjika.

  Baraza hilo lililoketi katika kikao chake cha dharura juzi Jumapili mjini Unguja, liliamua pia kusitisha uanachama wa baadhi ya watendaji wake waandamizi, kutoa karipio kali na kuwafukuza baadhi yao.

  Mtatiro, ambaye pia huandika uchambuzi katika gazeti hili amekubali uteuzi huo na kwamba hawezi kukwepa majukumu hayo muhimu.

  Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui amesema katika kutekeleza jukumu hilo, Mtatiro atasaidiana na Katani Mohamed Katani na Severina Mwijage.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku