Aug 21, 2016

Katiba Mbovu Inaibeba Serikali Kufanya Maamuzi Yenye Msukumo wa Kichama zaidi

Bunge la Tanzania
KATIBA ya Tanzania ni mbovu. Hali hiyo imekuwa ikitumiwa na serikali kufanya uamuzi wenye msukumo wa kichama zaidi, Faki Sosi.

Harold Sungusia, Wakili na Mwanaharakati wa Haki za Binaadamu Tanzania amesema kuwa, zuio la mikutano ya vyama vya siasa nchini lililotolewa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) linatokana na kutokuwa na Katiba nzuri.

Amesema kuwa, kutokana Katiba yetu, rais aliyepo madarakani ndiye anayeteuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) na makameshna wengine wa tume ambao hutokana na itikadi yake.

“Angalia mazingira haya, rais anayetokana na chama cha siasa ndiye anayeteua Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi.
“Hawezi kumteua mtu ambaye hawafanani itikadi, sasa katika mazingira haya unategemea nini wakati wa uchaguzi?” amehoji.

By  Faki Sosi.

Install SIASA HURU App Kwenye Simu Yako Kusoma Habari hizi Kirahisi, Bonyeza HAPA

Post a Comment

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © Siasa Huru l Habari za Siasa | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by SiasaHuru.com