Aug 12, 2016

Kigwangalla Kuipiga Nyundo Taasisi Hii Kwa Kuhamasisha Ushoga Tanzania

Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamis Kigwangala, amelishutumu shirika la LGBT Voice Tanzania kutumia mitandao ya kijamii kuhamasisha mapenzi ya jinsia moja jambo ambalo halivumiliki.

Dk. Kigwangalla amemtaka kiongozi wa taasisi hiyo, James Wandela Ouma kufika katika ofisi yake akiwa na nyaraka halisi za usajili ikiwemo cheti cha usajili, katiba na orodha ya wanachama, taarifa ya miradi inayotekelezwa na shirika hilo, walengwa wa miradi, wafadhili na wadau wanaoshirikiana nao.

“Ikumbukwe kwa kushidwa kufanya hivyo, kutapelekea kuchukuliwa hatua kali za kisheria. Pia napenda niombe jamii kutoa taarifa kwa mamlaka zinazosimamia sheria pale ambapo wanabaini vikundi vya watu, mtu au taasisi zinahamasisha mapenzi ya jinsia moja,” amesema Kigwangalla.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR