• Breaking News

  Aug 20, 2016

  Kijana Aliyedanganya Kuwa ni Mzee Akamatwa Marekani

  Shaun "Shizz" Miller amekuwa mafichoni tangu mwezi Aprili
  Polisi nchini Marekani wamemkamata mtoro mmoja baada ya kugundua kuwa alikuwa akidanganya kuwa yeye ni mtu mzee.
  Polisi walizingira nyumba moja huko Massachusetts na kumuamrisha Shaun "Shizz" Miller atoke nje.

  Kisha akatoka nje akiwa amejibadilisha na kuwa kama mtu mzee, lakini wakati polisi waligundua kuwa alikuwa ni yule walikuwa wakimtafuta mwenye umri wa miaka 31 walimkamata.

  Amekuwa mafichoni tangu ashtakiwe kwa kuhusika kwenye ulanguzi wa madawa ya kulevya mwezi Aprili.

  Wakati polisi walisaka nyumba hiyo walipata bunduki mbili na karibu dola 30,000 pesa taslimu.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku