Aug 17, 2016

KIMENUKA:Waliotafuna Fedha za Mikopo Wapewa Siku Saba Kuzirejesha


Wafanyakazi wa Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu (HELSB)na wa vyuo vilivyohusika kufanikisha malipo ya fedha za mikopo kwa wanafunzi hewa kuchukuliwa hatua kali za kisheria pamoja na kurudisha fedha zilizochukuliwa na wanafunzi hao.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Joyce Ndalichako .

“Kutokana na mambo yaliyobainika serikali imechukua hatua ikiwemo kuvitaka vyuo vikuu vilivyopokea fedha za wanafunzi ambao hawapo chuoni vinatakiwa virejeshe fedha hizo ndani ya siku Saba kuanzia leo, ” amesema.

Amesema vyuo vinatakiwa kuweka mfumo mzuri wa kuhifadhi kumbukumbu za wanafunzi kuanzia usajili, matokeo ya majaribio na ya mitihani na namba za akaunti za benki ambazo fedha za mikopo hulipwa ili kuondoa udanganyifu.

“Bodi ya mikopo inapaswa kuchambua na kuingiza mara moja mabadiliko ya taarifa zote za wanafunzi kama zilivyopokelewa kutoka vyuoni ili kuepusha ulipaji wa fedha kwa wanafunzi wasiostahili,” amesema


Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR