• Breaking News

  Aug 14, 2016

  KRC Genk yalazimishwa sare nyumbani, Samatta akitokea benchi

  KRC Genk wakati wanasubiria kucheza mchezo wao wa mchujo wa mwisho ili kufuzu Europa League hatua ya Makundi, usiku wa August 13 ilicheza mchezo wake wa tatu wa Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya klabu ya Waasland Beveren katika uwanja wa Luminus Arena.

  Huu ulikuwa ni mchezo wa tatu kwa KRC Genk kucheza toka kuanza kwa Ligi Kuu Ubelgiji msimu wa 2016/2017, wakiwa wameambulia ushindi mchezo wa kwanza na kufungwa mchezo wa pili ugenini na August 13 2016 ililazimishwa sare ya goli 2-2 dhidi ya Waasland Beveren, huku mshambuliaji wao mtanzania Mbwana Samatta akiingia dakika ya 47 kuongeza mashambulizi.

  Magoli ya KRC Genk yalifungwa na mshambuliaji wao raia wa Ugiriki Nikolaos Karelis dakika ya  35 baada ya kuwa nyuma kwa goli 2-0, lakini goli lao la kusawazisha Laurent Jans wa Waasland Beveren alijifunga dakika ya 73, magoli ya Beveren yalifungwa na Ibrahima Seck dakika ya 6 na Jonathan Buatu dakika ya 23.

  Kwa matokeo hayo Genk inakuwa nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu Ubelgiji yenye timu 16, huku ikiwa na jumla ya point nne katika michezo yake mitatu iliyocheza, Genk itarudi uwanjani August 18 2016 kucheza mchezo wake wa Europa League dhidi ya Lokomotiva Zagreb ya Croatia na mchezo wake wa nne wa Ligi Kuu Ubelgiji itacheza dhidi ya Lokeren ugenini August 21.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku