• Breaking News

  Aug 15, 2016

  Kunani kati ya AT na Peter Msechu! Bifu?


  Mkali wa muziki wa mduara Bongo, AT amemtupia maneno ya kejeli na lawama msanii mwenzake Peter Msechu.

  Haijulikani kwanini ameamua kuandika hivyo lakini kuna kila dalili kuwa Msechu aliongea kitu sehemu kilichomkera muimbaji huyo.

  “Mvuto Sifuri Bikaka @peter_msechu Nene km Lori Hivi kuongelea wembamba wangu unalipwa sitaki shobo km lakufanya huna jikate minyama yako ujichome mishkaki usi nitekenye mdomo ukataka niongee,” ameandika AT kwenye Instagram.

  “Tumbo Tumbo km Umeficha Kobe wewe nipotezee usilazimishe mimi niwe karibu na wewe sina shida ya kukuazima tumbo nende nalo harusini Mifulana km Turubali za Msimbani Babu kaa mbali na mimi kwani hivi na wewe ni msanii wanchi hii au Muuza kufia za Oliva Mtukuzi?”

  “Pyuuuuuuuuuuuuu ukiona nipo kimya ujue sihitaji varangati na mtu kiki zime adimika huna utakapopatia usinione Mwembamba ingia 18 uhadithie wenzio Mr Machupi ya kushonesha.”

  Tunafanya jitihada za kumpata Msechu kujua nini chanzo cha maneno hayo ya AT kwake.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku