• Breaking News

  Aug 16, 2016

  Kundi la orijino Komedi kukiona chamoto kwa kuvaa sare za Jeshi la Polisi kwenye Sherehe ya Harusi ya Masanja Mkandanizaji.


  Kundi la orijino Komedi kukiona chamoto kwa kuvaa sare za Jeshi la Polisi kwenye Sherehe ya Harusi ya Masanja Mkandanizaji.
  Jambo ambalo ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za Nchi.
  Kwa mujibu wa Sheria ya kanuni za makosa ya Jinai, sura ya 16 na marejeo yake ya mwaka 2002, kifungu cha 178 (1) na (2) kinachozungumzia makosa dhidi ya sare za majeshi ya ulinzi na usalama, kinabainisha wazi kuwa ni kosa kisheria kwa mtu yeyote ambaye siyo mtumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama kuvaa mavazi yanayotumiwa au kushabihiana na sare za majeshi hayo bila kibali kutoka kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Kufuatia kitendo kilichofanywa na kundi la kisanii la “ Original Comedy” kuvaa mavazi yanayoshabihiana na sare za Jeshi la Polisi, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam linachukua hatua za kisheria dhidi ya wasanii hao.


  Tupe maoni yako kuhusu jambo hili

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku