Aug 15, 2016

KUSEMWA na Wanasiasa Kuhusu Kuikodi Yanga Kwasababisha Manji Kujiondoa Yanga

Baada ya headlines za muda mrefu kuhusu wazo la mfanyabiashara na mwenyekiti wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans Yusuph Manji kuomba ridhaa ya kuikodi klabu hiyo kwa kipindi cha miaka 10 kupingwa na baadhi ya watu.

Habari zilizoenea katika mitandao ya kijamii na baadhi ya watu wa ndani ya Yanga leo August 15 2016 ni kuwa mwenyekiti wao Yusuph Manji anajiondoa rasmi na kuachia nafasi ya uenyekiti wa Yanga kwa sababu ya maneno kuwa mengi na kudai kusemwa na wanasiasa kuhusu wazo lake.

Sababu mbili zinazodaiwa kumfanya Yusuph Manji amejiondoe  ndani ya Yanga ni kusemwa na baadhi ya viongozi wa serikali na baadhi ya viongozi wa Yanga ambao wanatajwa kutumiwa na baadhi ya wafanyabiashara kwa maslahi yao binafsi, bado Manji hajatangaza rasmi kupitia vyombo vya habari.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR