• Breaking News

  Aug 29, 2016

  Afya ya Lema Mbaya Baada ya Kususia Chakula Mahabusu

  Godbless Lema
  Afya ya Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema imeripotiwa kuwa mbaya baada kususia kula chakula akiwa mahabusu tangu alipokamatwa juzi asubuhi.

  Lema alikamatwa na polisi akiwa nyumbani kwake juzi alfajiri na taarifa za kukamatwa kwake zilithibitishwa na Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro ambaye hata hivyo hakutaja sababu za kukamatwa kwa mbunge huyo.

  Imeelezwa kuwa mbunge huyo tangu akamatwe na polisi amegoma kula chakula hali iliyopelekea afya yake kuwa mbaya  na amefanya hivyo kwa sababu anaamini anaonewa na hata kukamatwa kwake kulikuwa ni kwa kumdhalilisha.

  Bwana Calist Lazaro amesema Lema amekataa kula hadi hapo atakapopelekwa mahakamani na kuliomba Jeshi la Polisi kumuachia kwani akipata madhara matatizo mapya yanaweza kuzuka.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku