• Breaking News

  Aug 11, 2016

  List Mpya ya Wanasoka 10 Wanaolipwa Mkwanja Mrefu Duniani Hii Hapa

  Kwa mujibu wa mtatndao wa sokkaa.com, wachezaji wawili bora duniani Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wamewaacha wengine mbali katika kuvuta mkwanja mrefu kwa upande wa wacheza soka.

  Ronaldo, ambaye hivi karibuni ameisaidia Ureno kushinda kombe la mataifa ya Ulaya 2026, anaongoza chat hiyo akiwa na mshahara wa £288,000 kwa wiki baada ya makato ya kodi (sawa na kitita cha £15 million kwa mwaka) waka Messi akiwa nafasi ya pili kwa kulipwa vizuri anachukua kitita cha £275,000 (sawa na £14.5 million kwa mwaka).

  Baada ya kukamilika kwa dili lililovinja rekodi ya uhamisho duniani la ada ya paundi milioni 89 (sawa na dola za Marekani milioni 115.98), Paul Pogba ambaye amesaini miaka mitano kuitumikia Manchester United mkataba wake unamfanya alipwe £290,000 kwa wiki.

  10. David Silva (Manchester City)

  Mshahara wa kila wiki: £200,000

  Mshara kwa mwaka: £10.9 million


  9. Neymar (Barcelona)

  Mshahara wa kila wiki: £220,000

  Mshahara wa mwaka:£11.4 million  8. Asamoah Gyan (Shanghai SIPG)  Mshahara wa kila wiki: £227,000

  Mshahara wa mwaka: £11.8 million

  7. Sergio Aguero (Manchester City)


  Mshahara wa kila wiki: £240,000

  Mshahara wa mwaka: £11.9 million


  6. Yaya Toure (Manchester City)


  Mshahara wa wiki: £240,000

  Mshahara wake kwa mwaka ni: £11.9 million


  5. Zlatan Ibrahimovic (Manchester United)


  Mshahara wa wiki: £250,000

  Kwa mwaka anaingiza: £11.4 million  4. Wayne Rooney (Manchester United)


  Mshahara wa wiki: £260,000

  Kwa mwaka anavuna mshahara: £13 million


  3. Paul Pogba (Manchester United)


  Mshahara wa wiki: £290,000 (kabla ya makato ya kodi)

  Mshahara kwa mwaka:£13.9 million

  2. Lionel Messi (FC Barcelona)  Mshahara kwa wiki: £275,000 baada ya makato ya kodi

  Mshahara kwa mwaka: £14.5 million baada ya makato ya kodi

  1. Cristiano Ronaldo (Real Madrid)


  Mshahara kwa wiki: £288,000 baada ya makato ya kodi

  Mshahara kwa mwaka: £15 baada ya makato ya kodi

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku