• Breaking News

  Aug 16, 2016

  Maalim Seif agoma kumpa mkono Dk. Shein


  KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amekataa kusalimiana kwa kushikana mkono na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.

  Tukio hilo lilitokea jana mchana wakati wa mazishi ya Rais wa pili wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi, aliyezikwa jana katika makaburi yaliyoko maeneo ya Migombani visiwani hapa.

  Katika Uchaguzi Mkuu mwaka jana, Maalim Seif alishindana Dk. Shein ambaye aliibuka mshindi katika uchaguzi wa marudio wa Machi 20, mwaka huu.

  Hata hivyo, Maalim Seif alilalamikia ushindi wa Dk. Shein kwa kile alichosema haukuwa halali kwa kuwa alifanyiwa hujuma na kuporwa ushindi wake uliopatikana Oktoba 25 mwaka jana.

  1 comment:

  1. Shein tu hali hiyo je akikutana na Jecha

   ReplyDelete

  Siasa

  Michezo

  Udaku