• Breaking News

  Aug 13, 2016

  Maalim Seif Amtembelea Ndugai


  Dar es Salaam. Ujumbe wa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad umemtembelea Spika wa Bunge, Job Ndugai nyumbani kwake Salasala Dar es Salaam kumjulia hali baada ya kutoka India alikokwenda kuchunguzwa afya yake.

  Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza Rais Mstaafu wa Serikali ya Zanzibar,  ameambatana na Kaimu Mwenyekiti wa CUF, Severina Mwijage, Naibu Katibu Mkuu CUF Tanzania Bara, Magdalena Sakaya na Naibu Katibu Mkuu mstaafu, Julius Mtatiro.

  Ndugai amemhakikishia Maalim Seif kuwa hali yake kiafya imeimarika sana.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku