Waliozoea kusafiri kwa mabasi kwa siku moja kutoka Dar es salaam kwenda Mbeya na kutoka Dar es salaam kwenda Mwanza na kwingineko kwenye umbali sawa na huo, sasa inabidi wajipange kisaikolojia kutumia siku mbili kukamilisha safari hizo. Hayo yamebainishwa na Meneja Usalama Barabarani na Mazingira wa SUMATRA, Geofrey Silanda. Uamuzi huo umetokana na utafiti uliofanywa na mamlaka hiyo na kubaini kwamba mabasi yanayofanya safari kwenye mikoa hiyo hayapaswi kusafiri kwa siku moja.

Toa maoni yako


Post a Comment

 
Top