Aug 13, 2016

Magufuli: Kuna Viongozi wa UVCCM Wamegawana Magorofa ya Vitega Uchumi ya Umoja Huo

Mwenyekiti wa CCM Mh. John Pombe Magufuli akihutubia wanachama wa chama hicho leo kwenye ofisi ndogo ya CCM Lumumba amesema, ana taarifa viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM UVCCM wamejigawia vyumba vya magorofa ya vitega uchumi wa umoja huo yaliyojengwa karibu na jengo la umoja wa vijana.

Amesema viongozi hao wamekuwa wakikusanya kodi za majengo hayo na kodi hizo kuishia mifukoni mwao.

Kazi ya kutumbua majipu ya chama ndio kwanza inaanza.

Source: ITV.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR