• Breaking News

  Aug 2, 2016

  Mahakama yatupilia mbali kesi ya kuharibu mali iliyokuwa ikimkabili Mbunge wa Arumeru Mashariki.


  Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Arusha imetupilia mbali kesi ya  kuharibu mali iliyokuwa inamkabili Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari pamoja na madiwani ishirini na tisa wa halmashauri ya Meru.

  Akitoa maelezo kabla ya kutamka kuifuta kesi hiyo Hakimu wa Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Arusha Desdery Kamgisha amesema  Mahakama imeamua kuondoa shauri ilo baada ya upande wa Jamhuri kuleta ombi  chini ya sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai namba 91 kifungu kidogo cha kwanza cha mwaka 2002.

  Hakimu Kamugisha amesema  ombi la upande wa Jamhuri limetoa ufafanuzi kwanini haitaweza kuendekea na kesi hiyo na kwakuzingatia ombi ilo mahakama imefuta shitaka ilo hivyo watuhumiwa wote wapo huru.

  Akizungumza nje ya Mahakama mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari amsema kesi hiyo ilikuwa na lengo la kupunguza kasi ya utendaji wao.

  Kwa upande wake Wakili wa upande wa utetezi Charles Abraham amesema amefurahishwa na uamuzi huo kwakuwa wateja wake wataendelea na kazi ya kutumikia jamii na wananchi wa Meru wamesema sasa mioyo yao imepata faraja.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku