• Breaking News

  Aug 10, 2016

  Majaliwa Ashtukia Ufisadi Mbeya


  Sakata la ufisadi katika ujenzi wa Soko Kuu la Mwanjelwa jijini hapa limechukua sura mpya baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kumwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukagua gharama za ujenzi na watakaohusika wasakwe mahali popote walipo hata wakiwa nje ya nchi.

  Majaliwa alitoa agizo jana asubuhi alipozungumza na wananchi waliofurika katika eneo la soko hilo muda mfupi kabla ya kurejea Dar es Salaam akimtaka CAG akague kujua sababu za kuongezeka kwa gharama za ujenzi kutoka Sh13 bilioni hadi Sh26 bilioni.

  “Soko hili lilitakiwa likamilike kwa gharama ya Sh13 bilioni, lakini watendaji wetu walifanyafanya mambo yao kwa kuingiza mikataba ya ovyo… kama hiyo haitoshi wakafanya tena mikataba ya ovyo hadi zikafikia Sh19 bilioni, bado tena wakarudia tena mikataba ya ovyo ikapanda gharama ya Sh23 bilioni,” alisema Majaliwa na kuongeza:

  “Lakini hapa karibuni katika umaliziaji napo wakafanya mikataba ya ovyo na gharama ikapanda hadi Sh26 bilioni. Nasema hivi hatuwezi kuwavumilia hawa, lazima watafutwe hata kama wapo nje ya Mbeya au nje ya nchi.”

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku