• Breaking News

  Aug 9, 2016

  Majambazi Yavamia Kambi ya Masista Igunga...

  Masista wa shirika la mtakatifu Yoseph wa kruni katika Parokia ya Mwanzugi wilayani Igunga wamevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia tarehe 8/8/2916.

  Katika uvamizi huo, majambazi walimjeruhi mlinzi na wakafanikiwa kuingia katika nyumba ya masista hao na kuwapigapiga masista na kuwanyanganya kamera iliyokuwa ikitunza kumbukumbu nyingi za shughuli zao pamoja na pesa taslimu sh.100,000

  Uvamizi huu ni wa Mara ya  nne sasa kiasi cha kuwakatisha tamaa madada hao ambao wana umuhimu wa pekee katika Huduma wanazotoa kwa wananchi/jamii inayozunguka parokia hii ya Mwanzugi.

  Pamoja na jitihada za wananchi wa Mwanzugi za kufuatilia mienendo ya majambazi hao, wamekuwa  mara kwa mara wakikosa nguvu kwa kutokuwepo kituo cha polisi eneo hili ambalo Lina wakazi wengi.

  Hata msaada wa kipolisi unapohitajika, hucheleweshwa hivyo kutoa mwanya kwa majamabazi hao ambao huja na silaha za moto kufanya shughuli za bila taabu.

  Ombi kwa mkuu wa Wilaya ya Igunga kutoka kwa wananchi wa Mwanzugi ni kuwawahakikishia usalama masista hawa kuliingana na Huduma wanazozitoa kwa wananchi wengi wa Igunga.

  Huduma wanazozitoa ni pamoja na matibabu na shule.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku