• Breaking News

  Aug 17, 2016

  Mamlaka ya Bandari Nchini TPA Imesema Inakabiliwa na Upungufu wa Mizigo

  Mamlaka ya Bandari nchini TPA imesema inakabiliwa na upungufu wa mizigo ambapo sasa kwa siku inahudumia magari 1500 tu tofauti na uwezo wake wa kuhudumia magari 3500 kwa siku yatokayo nje ya nchi na kuwa kutokana na hali hiyo hawawezi kupeleka magari kuhifadhiwa bandari kavu kwani hata yenyewe haina mzigo wa kutosha.

  Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Deusdedit Kakoko amesema hayo baada ya kumalizika kikao kilichoitwa cha ndani kati yake na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari nchini kilicholenga kujua hali halisi ya bandari ilivyo na mipango yake ya kuiboresha.

  Aidha mkurugenzi mkuu huyo wa mamlaka ya Bandari amesema kulikuwepo na udanganyifu katika utoaji wa mizigo bandarini kwa baadhi ya mawakala wa forodha ambao mzigo wa kupeleka nje ya nchi ulikuwa ukiuzwa hapa nchini kitu ambacho kimekanushwa vikali na chama cha mawakala wa forodha.

  Awali katibu wa jukwaa la wahariri Neville Meena amesema walifika bandarini hapo na kufanya kikao cha ndani na uongozi wa bandari hiyo baada ya kuwepo alichokiita mtikisiko katika utoaji wa huduma katika mamlaka ya bandari nchini.

  Chanzo: ITV

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku