• Breaking News

  Aug 10, 2016

  Mashabiki Naomba Mnisamehe - Emmanuel Mbasha

  Akizungumza na EATV kipindi cha FNL, Mbasha amesema hapendi kuzungumzia mambo yake na Flora Mbasha kwa sababu tayari Mungu amemshindia kesi ya ubakaji iliyomkabili na baadaye akaweza kushinda hivyo hapendi kumzungumzia tena mambo hayo.

  ''Kesi nimeshinda na amenishindia Mungu hivyo sipendi kuzungumzia mambo hayo tena, na hata wanasheria wangu wamenishauri nisizungumzie tena mambo hayo, ila kikubwa ninachowaomba mashabiki wafuatilie sasa ni nyimbo yangu mpya ya 'Haribu Mipango ya Shetani'' ambayo imetengenezwa na mtayarishaji wa nyimbo Pablo.

  Aidha Msanii huyo amesema hajarudiana na Flora Mbasha na yupo Single kwa sasa na anachokifanya kikubwa kwa sasa ni kumtumikia Mungu.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku